top of page
Search
esscreativeandlega

ESS Creative and Legal Foundation Yakutana na Umoja wa Mataifa

Na Erick Mukiza, Mkurugenzi Mtendaji wa ESS


Mnamo tarehe 20 Julai 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa ESS Creative and Legal Foundation, Bwa. Erick Mukiza, alikutana na Mwakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvalo Rodriguez. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Bwa. Mukiza alielezea kwa Bw. Rodriguez kuhusu kazi ya ESS Creative and Legal Foundation. ESS ni taasisi ya kutoa huduma za kisheria nchini Tanzania. Inatoa huduma mbalimbali za kisheria kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, wanawake, na vijana.

Bw. Rodriguez alisifu kazi ya ESS Creative and Legal Foundation. Alisema kwamba ESS inachangia katika kuboresha upatikanaji wa haki za kisheria nchini Tanzania.


Mazungumzo yalikua ya kirafiki na yenye manufaa. ESS na Umoja wa Mataifa wataendelea kufanya kazi pamoja ili kuboresha upatikanaji wa haki za kisheria nchini Tanzania.

3 views0 comments

Comments


bottom of page